Chelsea iko nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu ya England ikiwa na pointi zake 73 na imepania kuchukua ubingwa msimu huu.
Ukiachilia kusaka ubingwa mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ametoa kiasi cha pauni milioni 17.1 na kununua hotel ya kifahari nchini Israel ili aigeuze makazi yake pindi anapokwenda huko.
Raia huyo wa Urusi amenunua hotel hiyo ijulikanayo kama Varsano Hotel iliyopo katika mji wa Tel Aviv yenye mita za mraba 1,500 ambayo ina kila kitu ndani yake.
No comments:
Post a Comment