MAMA SALMA KIKWETE:RUSHWA YA NGONO HUPUNGUZA UFANISI KAZINI
Chama cha
majaji wanawake tanzania (Tawja) kimeiomba serikali na wadau wengine nchini
kushirikiana ili kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa
ya ngono.
Akizungumza
wakati akifungua warsha ya wadau wa utoaji haki juu ya kutokomeza matumizi
mabaya ya madaraka na rushwa ya ngono yaliyofanyika jijini Dar es salaamu mke wa
rais,Mama Salma Kikwete amesema rushwa ya ngono mahala pa kazi hupunguza kwa
kiasi kikubwa utendaji na ufanisi na kutaka adhabu kali kutolewa kwa wale wote
watakaobainika kufanya vitendo hivyo vya udhalilishaji wa
kijinsia
Naye
mwenyekiti wa chama cha majaji wanawake Tanzania (Tawja) Jaji Engera Kileo
amesema rushwa ya ngono mbali na kusababisha adhari za kisaikolojia pamoja na
udhalilishaji utu wa mwanamke pia inasababisha maambikizi ya ukimwi na kubaini
changamoto zinazowakabili ni pamoja na waathirika kuogopa kuweka wazi
wanapoombwa rushwa ya ngono.
No comments:
Post a Comment