Picha 8 za utengenezwaji wa video mpya ya Chidi Benz toka aache dawa za kulevya
Ni wiki kadhaa zimepita toka rapper Chidi Benz anaeiwakilishwa Ilala 88.5 Dar es salaam kutangaza kwenye exclusive interview na XXL ya Clouds FM kwamba ameamua kuacha utumiaji wa dawa za kulevya ambazo kwa kiasi kikubwa zilimrudisha nyuma kimaendeleo na hata kuwa mgomvi.
Baada ya kusema hayo siku hiyohiyo aliachia single mpya inaitwa ‘nakaza roho’ ambayo inaendelea kupata airtime kubwa kila siku kwenye radio huku ikingoja video yake.
Kupitia millardayo.com Chidi amezitoa pichaz za video ya single nyingine aliyofanya na Nonini inaitwa ‘how we get down’ aliyoifanya Nairobi wakati alipokwenda kupata matibabu yaliyomwezesha kuacha matumizi ya dawa za kulevya.
Chidi anakwambia alikua anapiga showz kila wiki na inambidi apumzike nyumbani labda kwa siku mbili tu lakini nyingine zinazobaki anakua mikoani kwenye showz zilizokua zinamuingizia mamilioni ambayo baadae yaliyeyuka kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment