China imekua na sheria kali sana kuhusiana na matumizi ya dawa za kulevya na endapo itathibitika mtu kukutwa na hatia hiyo mara nyingi hukumu yake huwa ni kifo ama kufungwa maisha.
Unakumbuka ile taarifa ya mtoto wa mwigizaji mkongwe maarufu duniani Jackie Chan kuhusishwa na matumizi ya dawa za kulevya? mahakama imekuja na taarifa hii baada ya kufanya uchunguzi.
Jaycee Chan ambaye ni mtoto wa mwigizaji huyo amekutwa na hatia mahakamani baada ya kukutwa na dawa hizo kinyume na sheria.
Mtoto huyo mwenye miaka 32 alifungwa mapema mwaka huu huko Beijing China baada ya kukutwa na dawa hizo huku polisi wakiendelea kufanya uchunguzi na sasa kisheria huenda akatumikia kifungo cha zaidi ya miaka mitatu jela.
Polisi walisema walikuta zaidi ya gram 100 za Marijuana katika nyumba ya mwigizaji huyo.
Awali baba wa mtoto huyo aliomba radhi na kusema tukio hilo limemsononesha na kumnyima raha.
No comments:
Post a Comment