Ángel Fabián Di María Hernández ni staa wa soka aliezaliwa miaka 26 iliyopita huko Argentina ambae kuanzia mwaka 2005 mpaka sasa ameshachezea club 4 za soka ambazo ni Rosario Central kuanzia 2005 – 2007, Benfica 2007-2010, Real Madrid 2010 – 2014 na sasa yuko Manchester United.
Taarifa ninayotaka kukupa ni kwamba staa huyu ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Argentina 2014 anaecheza nje ya nchi yake ambapo kwenye tuzo hizo zinazotolewa na Waandishi wa habari za michezo, Angel alikua anashindana na Lionel Messi and Sergio Aguero.
Unaambiwa hii ni mara ya kwanza kwa Lionel Messi kuikosa tuzo hiyo ambayo amekua akiichukua toka mwaka 2006.
No comments:
Post a Comment