Breaking News
recent

DEMBA BA KUTIMKIA BESIKTAS

KLABU ya Besiktas ya Uturuki imethibitisha kuwa Chelsea imepanga kumuuza mshambuliaji wake Demba Ba. Toka alipojiunga na Chelsea katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari mwaka 2013 akitokea Newcastle United, nyota huyo wa kimataifa wa Senegal amefunga mabao 14 katika mechi 51 alizovaa jezi ya Blues. Nyota huyo ameshindwa kutamba mbele ya Fernando Torres na Samuel Eto’o na ujio wa mshambuliaji mpya Diego Costa kutoka Atleico Madrid ndio uliomfugulia milango ya kutafuta klabu mpya huku meneja Jose Mourinho akiwa tayari kupokea kitita cha paundi milioni 10 kwa mauzo yake. Mwenyekiti wa Besiktas Fikret Orman amesema pamoja na kwamba Chelsea waliweka dau la paundi milioni 10 lakini wamefanikiwa kuwashawishi na kuteremsha kiwango hicho. Orman aliendelea kudai kuwa wataufahamisha uma mara watakapomaliza hatua za mwisho za usajili huo.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.