Breaking News
recent

BIRDMAN NA CASH MONEY WASHTAKIWA KWA KUKWEPA KULIPA WASANII WALIO TUMIA NYIMBO ZAO.

Lebo ya Cash Money na bosi wao Birdman wameshtakiwa kwa kukwepa kulipia Sample za nyimbo walizotumia kwenye kazi za wasanii wao.
Baada ya kusaini dili na kampuni ya Apple kutayarisha documentary ya Cash Money, Birdman ameshtakiwa na mwandishi mkongwe wamuziki akidai kuwa anatakiwa kulipwa dola milioni $3.3.
Sample za kazi za mwandishi huyu zilitumika kwenye kazi za Lil Wayne “Certified” na “You” na mpaka sasa Cash Money hawajalipia sample hizo.
Hili ni tatizo lingine kubwa kwa Birdman ambaye kwa sasa Lil Wayne nae anamdai dola milioni 51.
Mwezi February mwaka huu Cash Money walitakiwa kulipa dola milioni 1.1 kwa kampuni ya Orange Factor Music ikiwa ni ada ya nyimbo za Jay Sean zilizochezwa radio wakatu yupo na Cash Money.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.