Kama hujui hii ndio list ya mastaa wa kike watano wanaofanya muziki walioongoza kwa kuingiza mkwanja mkubwa kwa kipindi cha mwaka 2013-14 Marekani.
No.1- Beyonce: Mauzo ya Albam yake aliyoitoa kwa sapraiz mwaka 2013, mkwanja alioukusanya katika show zake unakadiriwa kuwa dola bil. 2.4 kwa show ya jiji moja, na hesabu zimeonyesha ameingiza jumla ya dola milioni 115 na kuwa mwanamuziki aliyezalisha pesa nyingi zaidi kwa mwaka 2014.
No.2- Taylor Swift: Huyu ni msanii wa kike pekee ambaye mauzo yake yanaweza kugonga platinum kwa mwaka huu, na akikusanya na pato lake kwenye mfuko wa kutangaza bidhaa, anakuwa na jumla ya dola milioni 64 mwaka huu.
No. 3- Pink: Huenda asiwe moja kati ya maarufu waliotawala mainstream, lakini lundo la cash anayoikusanya ‘kimyakimya’ inafikia kiasi cha dola milioni 52 kupitia show zaidi ya 85 ambazo zimemuingizia kama dola mil. 1 kwa kila show, na kitita kingine safi akijipatia kupitia madili yake ya matangazo ya bidhaa.
No. 4- Rihanna: Dada lao amekunja mkoba wa kushiba kupitia madili anayofanya na makampuni mbalimbali ya fashion, pamoja na kitita alichokikusanya kwenye tour aliyofanya na Eminem, mwaka huu hajaingiza albamu sokoni kwa hiyo kumbe bila kuimba muziki bado Rihanna anaweza kuzalisha pesa nyingi kutoka upande mwingine.
No. 5- Katy Perry: mkali wa rekodi ya “Dark Horse”, mauzo ya tiketi za show zake sehemu mbalimbali duniani, na mkwanja wa deal za matangazo umemfanya akusanye jumla ya kiasi cha dola mil. 40.
Wapo mastaa ambao wana majina ambayo yanasikika sana kama Nick Minaj hawajaweza kuingia hata kwenye top five ya wale walioingiza mkwanja mkubwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment