Unapozungumzia suala la majeraha ya wachezaji bila shaka mashabiki wa Manchester United wanapata homa ya ghafla .
Hii ni kwa sababu timu hii imekuwa na orodha isiyoisha ya wachezaji wenye majeraha .
Mbaya zaidi ni kwamba kila orodha hii inapoonyesha dalila za kungua mchezaji mwingine anaemia na inazidi kuwa ndefu .
Orodha hii iliongezeka kwenye mchezo dhidi ya Hull City wakati ambapo kiungo mshambuliaji Angel Di Maria alipoumia misuli ya nyonga kwenye dakika ya 14 ya mchezo na kulazimika kutoka.
Bado haijafahamika Di Maria atakaa nje ya uwanja kwa muda gani lakini kwa kawaida jeraha kama hili huhitaji kati ya siku 7 mpaka 10 ili kupona na wakati mwingine kuendana na ukubwa wake linaweza kuhitaji muda mrefu zaidi .
Kwa jumla Jeraha la Di Maria ni jeraha la 41 kwa mchezaji wa Manchester United kwa msimu huu tangu kuanza kazi kwa kocha Mholanzi Louis Van Gaal .
Idadi hii ndio idadi kubwa ya majeraha kwa wachezaji kwa timu yoyote ya ligi kuu ya England msimu huu hali inayowafanya United waamini kuwa huenda timu yao ina mkosi wa aina Fulani.
No comments:
Post a Comment