mvua kubwa iliyonyesha morogoro usiku wa jana na leo
asubuhi hasa maeneo ya wilaya ya kilosa imesababisha kusimama kwa mawasiliano
katika wilaya hiyo, watu
wameshindwa
kusafiri baada ya daraja la dumila ambalo linalotenganisha wilaya
ya kilosa na mvomelo kujaa maji na makazi kadhaa kukumbwa na mafuriko,
hivyo magari yanayotoka Dodoma hayawezi kupita na yanayoelekea dodoma
pia hayawezi kupita
mmoja wa mashuhuda walioko katika eneo la daraja hilo amesema kuwa hali
ni mbaya na mafuriko yasambaa sehem zote na daraja linapoanzia
limemeguka na eneo kubwa limegeuka bahari huku kwa mbali wakionekana
wakiwa juu ya miti
No comments:
Post a Comment