HAWA NDIO MAWAZIRI WALIOTENGULIWA MAJUKUMU YAO
Kufuatia majadiliano yanayoendelea Bungeni kuhusu ripoti iliyotolewa na kamati ya ardhi maliasili na utalii, Rais Jakaya Kikwete ametengua majukumu ya mawaziri wanne wa wizara za Maliasili na Utalii,Mambo ya Ndani,Ulinzi na
Jeshi la kujenga Taifa,pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Kufuatia maamuzi hayo mawaziri wa Wizara hizo ambao ni Balozi Khamis Kagasheki,Shamsi Vuai Nahodha,Emmanuel Nchimbi na Mathayo David Mathayo wameondolewa rasmi nyadhifa zao za uwaziri katika wizara hizo hadi uamuzi mwingine utakapotangazwa na Rais.
Uamuzi huu wa Ris Kikwete umetangazwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akijibu hoja zilizotolewa na Wabunge.
No comments:
Post a Comment