Breaking News
recent

SENTENSI TANO KUHUSU KUTEKWA KWA WAZIRI MKUU WA LIBYA

 

Libya

Breaking news kutoka Tripoli Libya zinaamplfy kwamba Waziri mkuu wa nchi hiyo Ali Zeidani ametekwa kutoka kwenye hoteli ambayo amekua akiishi huku tukio hilo likiwa limefanywa na watu wasiojulikana.

Nakumbuka siku kadhaa baada ya Rais Gaddafi kuuwawa kinyama, Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe alisema dhambi kubwa ya Wanalibya kumuondoa madarakani kiongozi aliekua ameisaidia nchi hiyo, itawarudia vibaya na watamkumbuka sana Gaddafi…… na kweli toka Gaddafi ameuwawa miaka miwili iliyopita hali haijawa shwari kabisa.

Waziri mkuu wa Libya kutekwa Oct 10 2013Serikali ya Libya imethibitisha kutekwa kwa Waziri mkuu na walinzi wake wawili ambao badae waliachiwa na kwamba watu waliomteka waliingia sehemu aliyokuwemo baada ya kuvamia wakiwa na silaha ambapo mpaka sasa haijulikani wamempeleka wapi kiongozi huyu mkubwa wa Serikali.

Msemaji wa kikundi kilichomteka amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na ishu ya kukamatwa kwa kiongozi wa Al Qaeda Abu Anas al Libi ambae anadaiwa kuhusika na mashambulizi ya kigaidi kwenye balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998.

Mmoja wa walinzi wa Waziri mkuu amesema waliomteka ni Wanajeshi ambapo hili tukio limefanyika kimyakimya manake risasi hazikupigwa kabisa.

Abu Anas al Libi
Abu Anas al Libi
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.