Breaking News
recent

RAISI JAKAYA KIKWETE AKATISHA ZIARA NCHINI KUWAIT NA KURUDI BONGO



Raisi Jakaya Mrisho Kikwete, amekatisha ziara yake ya kikazi nchini Kuwait na anatarajiwa kurudi jijini Dar es salaam, ili kushughulikia tukio la kulipuliwa kwa kanisa la Mtakatifu Yoseph Mfanyakazi Olasiti jijini Arusha, lililokuwa lizinduliwe jana na balozi wa Vatican nchini Tanzania Askofu Francis Kadinda.
Akizungumza na Clouds Fm kutokea nchini Kuwait, Mkurugenzi wa kurugenzi ya mawasiliano ya Raisi Ikulu, Salva Rweyemamu amesema, Raisi amepata taarifa hizo mara baada ya kutua nchini humo jana na kusikitishwa na kitendo hicho alichokitaja kutaka kuvuruga amani na usalama wa Tanzania na watu wake.
Tukio hilo lililotokea jana jijini humo limesababisha mtu mmoja kuuwawa na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.