Lakini chini ya utawala mpya wa kocha Louis Van Gaal utaratibu huo wa Ferguson umebadilika na tayari mmoja wa makocha waliokuwa wamezoeshwa na Fergie kualikwa kunywa mvinyo ametoa malalamiko yake.
Akiandika makala yake yaliyochapishwa kwenye gazeti la Evening Standard, kocha wa West Ham Sam Allardyce amesema ameshangazwa na kusikitishwa na kitendo cha kocha wa Manchester United Louis van Gaal kutomualika kunywa mvinyo baada ya mechi kati ya timu zao wikiendi iiyopita.
“Siku zote nilipokuwa nikienda Old Trafford nilikuwa nikialikwa kwa ajili ya mazungumzo kidogo pamoja na kunywa mvinyo.
“Huu utamaduni uliokuwepo kwa makocha wa timu pinzani, ndio maana nilishangazwa na kusikitishwa nilipotaarifiwa kwamba hakukuwa na utaratibu ule tena baada ya mechi kuisha. Niliambiwa utaratibu ule haupo tena, ikanibidi kuondoka.” - Aliandika Alladayce.
SOURCE: MILLARDAYO.COM
No comments:
Post a Comment