Breaking News
recent

TAKWIMU ZINAZOONYESHA UBORA WA REAL MADRID KWA SASA

Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania bila ubishi wowote ndio klabu bora kwa sasa ulimwenguni kote , hii ni kutokana na aina ya matokeo ambayo wanayapata kwneye mashindano mbalimbali ambayo wanashiriki kuanzia ligi ya Hispania , Kombe la Mfalme , Ligi ya mabingwa barani ulaya na michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko nchini Morocco ambako mabingwa hao wa Ulaya wameingia hatua ya Fainali .

Jumla yote Madrid imeshinda michezo 21 katika mashindano yote rekodi ambayo wanazidi kuivunja huku kukiwa hakuna dalili zozote za timu hii kupata matokeo tofauti na ushindi huku wakiwa wamevunja rekodi ya kushinda mechi 18 mfululizo iliyowahi kuwekwa na Barcelona iliyokuwa chini ya Mholanzi Frank Rijkaard katika msimu wa mwaka 2005/06.

Kwa kasi hii rekodi pekee ya kushinda mechi mfululizo iliyobaki kuvunjwa itakuwa ile iliyowahi kuwekwa na Ajax Amsterdam kwenye msimu wa mwaka 1971/72 ambapo timu hiyo ilishinda michezo 26 .

Wachezaji wa Real Madrid wakiwa mazoezini. 
Ubora huu unaonekana kwenye matokeo unatokana na aina ya wachezaji ambaoReal Madrid inao wakiongozwa na mchezaji bora kwa sasa Cristiano Ronaldo .

Takwimu kadhaa zinaonyesha kuwa Real Madrid wamekuwa bora kwenye kila idara na ni vigumu sana kuwazuia .

Katika michezo 21 ambayo timu hii imecheza hadi kufikia sasa , imefanikiwa kufunga jumla ya mabao 79 , ikiwa imeruhusu kufungwa mabao 10 pekee .

Katika mabao hayo 79 ambayo Madrid imefunga jumla ya mabao 19 yamefungwa kwa kutumia mguu wa kushoto , mabao mengine 42 yakiwa yamefungwa kwa kutumia miguu ya kulia na mengine 15 yakiwa yamefungwa kwa kichwa .

Zaidi ya hapo , mabao 9 yamefungwa nje ya eneo la hatari au kisanduku cha penalty (penalty box) na mabao 70 yakiwa yamefungwa ndani ya eneo hilo na mabao 8 yamefungwa kwa njia ya adhabu ya mkwaju wa penati .

Katika kipindi hiki chote wachezaji kadhaa wamechangia katika mafanikio ambayo Real imeyapata kwenye michezo yake 21 ambayo imeshinda mfululizo kuanzia kwa Cristiano Ronaldo , Gareth Bale , Karim Benzema , James Rodriguez , Toni Kroos, Isco ,Sergio Ramos , Pepe ,na kipa Iker Cassillas ambaye hatimaye amerudisha hadhi yake iliyowahi kutishia kupotea chini ya kocha Jose Mourinho.


Nyuma ya mafanikio yote haya ni kocha Mtaliano Carlo Ancelotti ambaye amefanikiwa kuwafanya wachezaji wote wa Real Madrid kuwa kitu kimoja na kupambana mwanzo mpaka mwisho kuhakikisha wanatimiza lengo ambalo ni kujaribu kuibuka na ushindi kwenye kila dakika 90 wanazokuwa uwanjani dhidi ya wapinzani wa aina tofauti .

Kocha Mtaliano Carlo Ancelotti amefanya kazi kubwa ya kuifanya Real Madridkuwa timu bora barani Ulaya . 


TareheMpinzani(timu)MashindanoMagoli(real)Magoli(wapinzani)Umiliki MpiraUfasaha wa pasiPasiMashuti
16/09/14BasleChampions League5154.3590.3656017
20/09/14Deportivo la CorunaLa Liga8259.8391.7567915
23/09/14ElcheLa Liga5164.7490.9166020
27/09/14VillarrealLa Liga2049.7285.665027
01/10/14LudogoretsChampions League2160.9387.7754815
05/10/14Athletic BilbaoLa Liga5060.1286.7658919
18/10/14LevanteLa Liga5061.390.7263617
22/10/14LiverpoolChampions League3054.1788.3868012
25/10/14BarcelonaLa Liga3142.1985.3843111
29/10/14CornellaCopa Del Rey4173.2289.5875811
01/11/14GranadaLa Liga4066.7788.0662815
04/11/14LiverpoolChampions League1060.1390.9971015
08/11/14Rayo VallecanoLa Liga5143.8381.3843515
22/11/14EibarLa Liga4062.385.5155917
26/11/14BasleChampions League1053.3284.355436
29/11/14MalagaLa Liga2157.8688.447418
02/12/14CornellaCopa Del Rey5063.0889.7168010
06/12/14Celta VigoLa Liga3048.7881.7538917
09/12/14LudogoretsChampions League4061.779160019
12/12/14AlmeriaLa Liga4160.579.9145812
16/12/14Cruz AzulFIFA Club World Cup4058.2889
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.