Breaking News
recent

IFAHAMU TIMU YENYE MASHABIKI WENYE KELELE KULIKO WOTE NCHINI ENGLAND....

united fans


Utafiti uliofanyika kwenye timu za soka nchini England ukiwaangalia mashabiki wa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi hiyo umeonyesha klabu ambazo zina mashabiki wanaozipenda klabu zao kuliko wote.
Utafiti huo umeitaja Man United kuwa klabu ambayo mashabiki wake wanashangilia kwa kelele nyingi kuliko mashabiki wote hususan kwenye mechi za ugenini.
united fans
Pamoja na kutokuwa na mengi ya kushangilia baada ya timu yao kutofanya vizuri tangu alipoondoka kocha Sir Alex Ferguson bado mashabiki wa United wametajwa kuwa na sauti kubwa kuliko wapinzani  wao kwenye mechi za ugenini .
Mashabiki wa Liverpool wanawafuatia mashabiki wa United kwa kelele nyingi kwenye mechi za ugenini .
Mashabiki wa Liverpool wanawafuatia mashabiki wa United kwa kelele nyingi kwenye mechi za ugenini .
Utafiti huu umeonyesha kuwa mashabiki wa United wanawazidi mashabiki wa timu zaNewcastle United na Liverpool ambao wanafuatia kwenye nafasi ya pili na ya tatu kwa kelele zao wakati wakiwa wamesafiri kuitazama timu yao ugenini.
Klabu ya Arsenal imeshuka hadi nafasi ya saba hali ambayo huenda ikawa inachangiwa kwa kiwango kikubwa na mashabiki wa timu hiyo kuonekana wamemchoka kocha waoArsene Wenger ambaye hivi karibuni alionekana hakubaliki mbele ya mashabiki wa timu yake kiasi cha kutengeneza mabango ya kutaka aachie ngazi.
Mashabiki wa WestBrom  ndio wenye kelele chache kuliko mashabiki wote kwenye ligi kuu ya England .
Mashabiki wa WestBrom ndio wenye kelele chache kuliko mashabiki wote kwenye ligi kuu ya England .
Mashabiki wa timu zinazopambana kuepuka kushuka daraja kama vile Burnley naQueens Park Rangers kwa pamoja na West Bromwich Albion zimeoneka kuwa na mashabiki wasio na kelele wanapokuwa kwenye mechi za ugenini hali ambayo huenda ikawa inachangiwa na jinsi ambavyo timu zao zimeshindwa kupata matokeo mazuri ziwapo ugenini.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.