Breaking News
recent

KAMA UNA TABIA HII, USIJARIBU KUJIAJIRI KABLA HUJABADILIKA...

Kwa ulimwengu wa sasa, ajira zimekuwa ngumu mno na pia zimekuwa na usumbufu mwingi. Watu wengi wanatafuta kazi na nafasi za kazi ni chache. Hata walio makazini nao hawazifurahii kazi kama zamani, sasa hivi mazingira ya kazi yamekuwa magumu, maisha magumu na mishahara haitoshi.
  Kutokana na matatizo haya kimbilio pekee limekuwa ni kujiajiri. Ambao wanatafuta kazi na hawapati inawalazimu kuanza kuwa na mawazo ya kujiajiri. Waioajiriwa nao wanawaza kujiajiri ili kuondokana na manyanyaso ya kwenye ajira.
kujiajiri3
  Hata wewe una wazo hilo la kujiajiri ili na wewe uweze kuyatawala maisha yako. Ama umeshajiajiri ila bado mambo hayaendi kama ulivyodhani!
  Ukiwaangalia waliojiajiri ni wachache wenye mafanikio makubwa. Wengi wanaendesha tu maisha yao kwa kujiajiri kwao na wengine mambo yanazidi kuwa mabaya hata baada ya kujiajiri.
  Ni tatizo gani linatokea kwa hawa waliojiajiri wachache kupata mafanikio makubwa na wengi kuishia kusota? Kuna tabia moja ambayo watu wengi wanayo na hiyo ndio inayofanya watu washindwe kufanikiwa wanapojiajiri.
  Duniani kuna makundi mawili ya watu, kuna ambao wanaweza kupanga na kufanya kitu na kuna ambao wanaweza kufanya vizuri ila mpaka waambiwe wafanye.
kujiajiri
  Kujua wewe uko kundi lipi, tafakari maisha yako kwa muda na uangalie ni mambo gani unayoyafanya vizuri na unayopendelea kufanya. Yale uliypanga mwenyewe ama yale uliyopangiwa kufanya? Jiulize ni kitu gani kinakufanya uamke asubuhi na mapema? Ni kwa sababu hutakiwi kuchelewa kazini au kwa sababu unaamka kuianza siku yako na kuifurahia?
  Wanaoweza kufanya mambo yao wenyewe bila kuambiwa ni sehemu ndogo sana ya jamii na hawa ndio wanaofanikiwa kwenye ajira na hata nje ya ajira. Wanaokuwa wafanyakazi bora na wanaopandishwa vyeo ni wanaofanya tofauti na wengine.
kujiajiri2
  Wanaosubiri kuambiwa cha kufanya ni sehemu kubwa ya jamii na wengi wanaishia kuwa wafanyakazi wa kawaida na hata wakijaribu kujiajiri mambo yanazidi kuwa magumu.
  Kama wewe huwa unafanya jambo baada ya kuambiwa ufanye basi usikurupuke kujiajiri. Anza kujenga tabia ya kupanga na kufanya mambo yako mwenyewe bila hata ya kuambiwa. Kama umeajiriwa na unayajua majukumu yako basi wewe fanya kwa ufanisi na ubunifu mkubwa. Usiishie tu kufanya vile unavyoambiwa, nenda mbele na ongeza thamani zaidi. Kufanya hivyo kutakuongezea utaalamu na pia kutakupatia tabia ya kuweza kujiajiri. Ili uweze kufanya zaidi na kwa utofauti ni lazima utumie uwezo na vipaji vyako ulivyonavyo. Kila mtu ni mbunifu hivyo hutokosa cha kufanya.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.