Breaking News
recent
MAMA SALMA KIKWETE:RUSHWA YA NGONO HUPUNGUZA UFANISI KAZINI
 

Chama cha majaji wanawake tanzania (Tawja) kimeiomba serikali na wadau wengine nchini kushirikiana ili kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono.
Akizungumza wakati akifungua warsha ya wadau wa utoaji haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka na rushwa ya ngono yaliyofanyika jijini Dar es salaamu mke wa rais,Mama Salma Kikwete amesema rushwa ya ngono mahala pa kazi hupunguza kwa kiasi kikubwa utendaji na ufanisi na kutaka adhabu kali kutolewa kwa wale wote watakaobainika kufanya vitendo hivyo vya udhalilishaji wa kijinsia
Naye mwenyekiti wa chama cha majaji wanawake Tanzania (Tawja) Jaji Engera Kileo amesema rushwa ya ngono mbali na kusababisha adhari za kisaikolojia pamoja na udhalilishaji utu wa mwanamke pia inasababisha maambikizi ya ukimwi na kubaini changamoto zinazowakabili ni pamoja na waathirika kuogopa kuweka wazi wanapoombwa rushwa ya ngono.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.