Breaking News
recent

UTARATIBU MPYA WA KUJISAJIRI KWENYE SOCIAL NETWORK CHINA NI STORY YA NGUVU...

China News

Kuna watu ambao sio watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii, wapo ambao wanaandika lugha ambayo sio nzuri, hii inatokana na kutokuwepo utaratibu rasmi wa kujisajili kwa kutumia majina sahihi.
Tumeshuhudia account nyingi mitandaoni ambazo wanaoziendesha sio wahusika wenyewe, ziko zenye majina ya mastaa, viongozi, lakini ukweli ni kwamba wanaoziendesha sio wenye majina hayo.
China ni moja ya nchi ambazo zimefanikiwa kuzuia vitu vingi mitandaoni , safari hii utaratibu ambao wameutangaza utaratibu mpya, kama unafungua accountt yako kwenye mtandao wowote wa kijamii ikiwemo Weibo ambao uko kama Twitter, Blogs na mingineyo ni lazima ufungue kwa jina lako kamili, hakuna a.k.a hakuna nickname inayotakiwa.

Kama ikitokea ukafanya usajili kwa jina fake account yako itazuiwa na hutoweza kuitumia, wamefanikiwa kuzuia mengi na hii wanaamini watazuia ‘utapeli’ wa majina ya uongo ambayo yako mitandaoni.
Unaambiwa hata ukitaka kucomment chochote kilichoandikwa mtandaoni lazima ujisajili mtu wangu, hii kama ikija Bongo unaonaje labda?
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.