Breaking News
recent

KAMA UNAWEZA KUPATA KITU HIKI KILA SIKU BASI UNAWEZA KUPATA CHOCHOTE UNACHOTAKA MAISHANI..

Mara nyingi ninapokaa na kuyatafakari maisha yangu na ya jamii inayonizunguka huwa napata majibu ya ajabu sana. Majibu mengine huwa nadhani ni ya kipuuzi ila ninavyozidi kufikiri naona yanaleta maana kubwa sana.

maisha4

 Kwa mfano mimi binafsi sijawahi kuona mtu mzima aliekufa kwa njaa. Na pia sijawahi kusikia mtu amekufa kwa njaa dar es salaam ama maeneo mengine ya mjini.
  Na sehemu zote hizi ambazo watu hawafi kwa njaa bado wanalalamika maisha ni magumu sana.(na ili maisha yawe mazuri ni sharti yawe magumu) Katika maisha hayo magumu, mtu atakosa mavazi ya kuvaa, anakosa pakulala ila hatakosa kitu cha kula.
  Mtu kuhakikisha anapata chakula katika mazingira magumu aliyopo inatufundisha nini?
  Mtu yuko tayari kufanya chochote kuhakikisha anapata chakula. Na ni kwa sababu anajua asipopata chakula atakufa. Na hakuna anaependa kufa, japo maisha ni magumu.
  Kwa hiyo linapokuja swala la kifo binadamu wengi tunahakikisha tunafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuokoa maisha yetu. Hata kama tunalalamika kiasi gani, linapokuja swala la kifo kila mmoja wetu atahakikisha anazuia kisimpate.
  Kuweza kupata chakula hata mara moja katika mazingira magumu inaonesha kwamba binadamu tuna uwezo mkubwa ambao hatujaweza kuutumia ipasavyo. Na katika harakati hizo za kuokoa maisha kuna wengi wanatumia uwezo walionao vibaya, kama kuiba, kudhulumu ama kujipatia wanachotaka kwa njia yoyote ambayo sio halali.
  Kama kila mtu angeweza kutumia nguvu hii kubwa ananyoweza kuitumia kuokoa maisha yake katika mazingira magumu tungeweza kuyabadili maisha yetu kwa kiasi kikubwa sana.
  Kama kila mtu angeweza kutumia nguvu sawa na anayotumia kutafuta chakula, akatumia nguvu hiyo kwenye jambo lolote analotaka hakina angeweza kulifanikisha bila tatizo.
  Tatizo kubwa tunaridhika, tukishaona maisha yetu hayapo hatarini sana tunakubaliana na hali ya mambo na tunaendelea na maisha. Tukiona hatupati vile tunavyotaka, ambavyo haviwezi kuhatarisha maisha yetu kama tusipovipata, tunatafuta mtu wa kumtupia lawama.
  Tukishapata wa kulaumu(na lazima apatikane) tunaona yeye ndio mhusika wa kila kitu na sisi tunaendelea na maisha yetu kwenye mazingira magumu. Ugumu huo wa mazingira tunaweza kuubadili ila kwa vile tumeshatafuta wa kumlaumu hakuna lolote tunalofanya.(soma; usimlaumu yeyote)
  Wewe una nguvu kubwa sana liyopo ndani yako. Una uwezo mkubwa wa kupata chochote unachotaka na kuyabadili maisha yako. Unaweza kufanya hivyo kama utajua kwamba wewe ndio kiongozi mkuu wa maisha yako. Hakuna yeyote anayeweza kuyabadili maisha yako kama wewe mwenyewe hutochukua hatua ya kufanya hivyo.(soma; uchaguzi mkuu muhimu maishani mwako)
  Kama kila mtu anaweza kula katika mazingira yoyote magumu aliyopo basi anaweza kupata chochote hata kama mazingira ni magumu kiasi gani. Kinachotakiwa ni yeye tu kujua umuhimu wa anachokitaka na uwezo mkubwa ulio ndani yake.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.