Breaking News
recent

YAYA TOURE AJIANDAA KIKAMILIFU KWA MECHI YA UFUNGUZI DHIDI YA JAPAN...

article-0-1E9E0CC300000578-315_634x432
Majeruhi: Yaya Toure, akiwa mazoezini jumatatu, anaendelea kuimarika kwa kasi kuelekea mchezo wa ufunguz
On the ball: Toure in training
Recovery: Toure suffered a thigh injury in April
 KIUNGO wa Ivory Coast,Yaya Toure anaendelea kuimarika kwa kasi kuelekea katika mchezo wa ufunguzi wa kombe la dunia dhidi ya Japan jumamosi, amesema kocha Sabri Lamouchi.
Toure ameshindwa kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake tangu alipofanyiwa upasuaji mwezi uliopita.
Lamouchi amesema timu ya madaktari wa  Ivory Coast inajitahidi sana kuhakikisha mchezaji huyo bora wa mwaka wa Afrika anacheza wakati nchi yake itakapoanza mchezo wa ufungizi wa kundi C dhidi ya Japan mjini Recife.
‘Tunafanya kila linalowezekana ili acheze” kocha aliwaambia waandishi wa habari.
Toure alipata majeruhi katikati ya mwezi aprili mwaka huu, lakini alirudi uwanjani kuisaidia Manchester City kutwaa ubingwa wa pili katika misimu mitatu.
 
Halafu akaenda Qatar kwa ajili ya matibabu na baadaye alijiunga na kikosi cha Ivory Coast kwenye kambi ya mazoezi huko America.
Toure hakucheza mechi mbili za kupasha pasha dhidi ya Bosnia na El Salvador.
 
SOURCE: SHAFII DAUDA
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.